Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya kupambana na ugaidi nchini Iraq yameanza hatua mpya ya mapambano ya kukabiliana na vikundi vya kigaidi vya Daesh nchini humo, katika kuukomboa mji wa Musol.
Jumapili ya leo mmajeshi hayo yamefanya mashambulizi katika sehemu ya (Al-quds) iliopo katika mji wa Musol na kufanikiwa kwenda mbele katika sehemu hiyo, ambapo mpaka sasa mapambano yanaendelea baina ya kikundi cha kigaidi cha Daesh na majeshi ya Iraq katika sehemu ziliobaki ya sehemu hiyo.
Kikundi cha kigaidi cha Daesh kilikuwa kinaitumia sehemu ya Al-quds kuwa ni kama makau makuu ya kuandaa magari yaliotegwa mabomu, ili kufanya mashambulio ya kigaidi katima maeneo mbalimbali katika mji wa Musol.
Kala ya hapo majeshi ya Iraq yamefanikiwa kukomoa sehemu nyingi katika mji wa Musol kutoka mikononi mwa Daesh mjini humo.
Aidha kamanda wa jeshi la Iraq jana ametangaza kuangamia kwa makamanda wawili wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Musol.
“Abu Ayubu Al-Qurshiy” na “Abu Seifu” ambao ni katika makamanda wakubwa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh wameangamia kufuatia shambulio la anga liliofanywa na majeshi ya Iraq katika sehemu ya “Al-Quds” na Babul Tuba” katika mji wa Musol.
Mji wa Musol ni moja kati ya miji mikubwa nchini Iraq, ambapo uko kaskazini mwa Iraq ambapo mji huo mpaka sasa ni miaka miwili uko chini ya kikundi cha kigaidi cha Daesh.
mwisho/290
25 Desemba 2016 - 18:51
Msimbo wa Habari: 800727
Majeshi ya kupambana na ugaidi ya Iraq yamefikia ushindi mpya katika sehemu ya (Al-Qusi) baada ya kuikomboa sehemu hiyo kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Musol nchini Iarq